Hapa Kwetu JAPANI

Juni-gatsu ; Rogetsu (jina la zamani)


Januari


Koto hajime

 
Kuanza kutayarisha sherehe ya mwaka mpya


Nengajo-kaki

Mwisho wa mwaka watu wana shughuli nyingi sana.
Katika hizo shughuli, kazi moja kubwa ni kuandika kadi ya mwaka mpya inaitwa Nengajo.
Kwenye kadi wanawapa marafiki zao salamu pamoja na habari zake na za nyumbani. Mara nyingine inaweza kuwa hawajaandikiana mwaka mzima na wala hawajakutana miaka. Ndiyo maana watu wanapenda sana kuandikiana Nengajo. Zikiwa nyingi mtu mmoja anaweza kuandika kadi mia moja, mia mbili au zaidi.
Siku hizi watu wanapenda kuandika na kompyuta lakini wazee wanapenda ya mikono. Wanaotumia kompyuta mara nyingi wanaweka picha yake au ya watoto.
Siku hizi vijana wanaandikiana kadi za Krismas lakini wanapenda Nengajo zaidi na wanaandika nyingi zaidi.

Krismasi

Wakrist si wengi hapa Japani lakini watu wengi ambao si wakrist wanafanya sherehe nyumbani kwa sababu ya watoto.
Watoto wanapenda sana Krismas kwa kuwa wanamsbiri Father Christmas awaletee zawadi ya Krismas.
Mwezi wa Desemba madukani wanafanya Sale. Wakati huu akina mama na baba, au babu na bibi wanaenda madukani kutafuta zawadi za watoto au za wajukuu wao.
Siku ya Krismas wanafanya karamu nyumbani. Baada ya karamu watoto wanaenda kitandani. Lakini hawataki kulala usingizini. Wana hamu ya kumwona Father Christmas kwa macho. Hata siku moja hawaomwoni kwa macho kwa sabanu hata wazazi wao wako na macho wanasubiri watoto walale usingizini.
Baadaye wakishalala wazazi wanaenda kuwawekea zawadi chumbani.
Kesho yake ya Krismas watoto watakapoamuka wataziona zawadi zao na watajua kumbe Father Christmas amesha ondoka saa nying.

Mochi-tsuki

Siku ya mwisho mwisho ya mwaka tunatengeneza rice cake ambayo inaitwa Mochi.
Kwanza tunapika mchele kwa mvuke. Mchele si wa kupikia wali wa kawaida,
ni wa aina nyingine. Mchele ukiiba tutapeleka kwenye kinu kisha tutaponda na mchi mpaka kusagwa kabisa.
Kinu tunaita Usu kwa Kijapani na mchi unaitwa Kine.
Tukimaliza kupondaponda tunaviringanisha mochi. Tunapamba Mochi mbili na tutaweka chungwamoja juu ya mocjhi.
Hizo mochi tutaweka mpaka katikati ya mwezi wa Januali. Hii ni kama sadaka kwa Mungu.

Joya no kane

Kengele ya mwisho wa mwaka


Misoka-soba

Tambi